

Lugha Nyingine
Utalii wa anga ya juu wa China kufikia hatua ya awali ya kuwa wa kibiashara katika miaka 5-10 ijayo
Roketi iliyoboreshwa ya kubebea mizigo ya ZQ-2 Y-1 iliyobeba satalaiti mbili za majaribio ikirushuwa kutoka eneo la majaribio ya uvumbuzi wa vyombo vya anga ya juu vya kibiashara, kaskazini magharibi mwa China, Novemba 27, 2024. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)
BEIJING - Sekta ya utalii wa anga ya juu ya China inatarajiwa kufikia hatua ya awali ya shughuli za kibiashara ndani ya miaka mitano hadi kumi ijayo, sanjari na maendeleo ya haraka na endelevu ya tasnia ya vyombo vya anga ya juu ya nchi hiyo, jumuiya ya washauri bingwa ya serikali ya China imesema jana Jumanne.
Ripoti ya mapema mwezi Aprili kuhusu maendeleo ya sekta ya anga ya juu ya kibiashara nchini China kutoka kampuni ya ushauri ya CCID chini ya Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Upashanaji wa Habari ya China, imesema kuwa mnyororo mzima wa viwanda umepata ukuaji wa haraka.
Ripoti hiyo inapendekeza kwamba kufikia mwisho wa kipindi cha Mpango wa 15 wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa China (2026-2030), au katika kipindi chake cha mpango wa 15 wa miaka mitano (2031-2035), tasnia ya utalii wa anga ya juu ya nchi hiyo huenda itakuwa imekua zaidi, kuwa na uwezo wa kupata faida kubwa na kutambuliwa zaidi duniani.
Yang Shaoxian, mtafiti mkuu katika kamapuni hiyo ya ushauri ya CCID, anakadiria kuwa ndani ya miaka mitano hadi kumi ijayo, utalii wa anga ya juu na safari za mwezini za kibiashara za China zinatarajiwa kupata sera ya kuvunja wigo, kufaulu kupitia majaribio na kupata uthibitishaji, au kuingia katika kipindi cha mwanzo cha uendeshaji.
Sekta ya anga ya juu kibiashara ni yenye umuhimu wa kimkakati kwa China na imetajwa kuwa "injini mpya ya ongezeko la uchumi" katika ripoti ya kazi ya serikali ya mwaka 2024.
Ripoti hiyo ya kazi ya serikali ya mwaka huu pia imesisitiza umuhimu wa sekta hiyo, ikisema kuwa China itahimiza maendeleo mazuri na salama ya shughuli mpya zinazoibukia, zikiwemo za utalii wa anga ya juu wa kibiashara na uchumi wa anga za chini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma