Rais Xi atoa wito wa kuzidisha urafiki kati ya China na Malaysia

(CRI Online) April 16, 2025

Rais Xi Jinping wa China kwenye makala aliyoitia saini ameeleza kutarajia kukutana na marafiki wa Malaysia ili kusherehekea urafiki kati ya China na Malaysia na kupanga ushirikiano wa siku zijazo.

Rais ametoa kauli hiyo kwenye makala hiyo yenye kichwa cha "Meli ya Urafiki kati ya China na Malaysia Ielekee Mustakbali Bora Zaidi" iliyochapishwa katika vyombo vya habari vya Malaysia kabla ya kuwasili nchini humo kwa ziara ya kiserikali.

Amesema nchi hizo mbili lazima zifanye kazi pamoja ili kutoa kasi mpya kwa meli yao ya urafiki ambayo imepita mto mrefu wa historia, na kuhakikisha kwamba inasonga mbele kwa kasi kuelekea upeo mzuri zaidi.

Rais Xi pia ameeleza matumaini yake kwamba watu wa nchi hizo mbili watatembeleana mara kwa mara kama familia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha