Rais Xi Jinping awasili Kuala Lumpur kwa ziara ya kiserikali nchini Malaysia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 16, 2025

Rais wa China Xi Jinping akikaribishwa kwa furaha na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim na maofisa wengine waandamizi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

KUALA LUMPUR - Rais wa China Xi Jinping amewasili mjini Kuala Lumpur jana Jumanne kwa ziara ya kiserikali nchini Malaysia ambapo alikaribishwa kwa furaha na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur.

Katika taarifa yake ya maandishi alipowasili kwenye uwanja huo wa ndege, Rais Xi amesema anatarajia kuchukua ziara yake hiyo kama fursa ya kuzidisha zaidi urafiki wa jadi na kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa kwa pande mbili.

Rais Xi ametoa wito kwa pande hizo mbili kuhimiza ushirikiano katika jitihada za ujenzi wa mambo ya kisasa, kwa pamoja kuimarisha mawasiliano na kufundishana katika ustaarabu, na kuinua hatua kwa hatua ujenzi wa jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja kwenye kiwango kipya.

Ameelezea matumaini yake kuwa, kwa juhudi za pamoja za China na Malaysia, ziara yake hiyo itapata matokeo yenye matunda mengi, kufungua ukurasa mpya wa kihistoria wa urafiki wa ujirani mwema na kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na kuingia katika "Miaka 50 ya Dhahabu" kwa uhusiano wa pande mbili.

Rais wa China Xi Jinping akiwasalimia   watu wanaomkaribisha wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

Rais wa China Xi Jinping akiwasalimia watu wanaomkaribisha wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

Wasanii  wakicheza ngoma ya jadi ya simba kumkaribisha Rais wa China Xi Jinping mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Yu Dongsheng)

Wasanii wakicheza ngoma ya jadi ya simba kumkaribisha Rais wa China Xi Jinping mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Yu Dongsheng)

Ndege iliyombeba Rais wa China Xi Jinping ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

Ndege iliyombeba Rais wa China Xi Jinping ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

Watu wakimkaribisha Rais wa China Xi Jinping mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Yu Dongsheng)

Watu wakimkaribisha Rais wa China Xi Jinping mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Yu Dongsheng)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha