Rais Xi asema uhusiano kati ya China na Vietnam umekita mizizi, kudumishwa na kuwezeshwa na watu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 16, 2025

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akitoa hotuba kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano  huko Hanoi, mji mkuu wa Vietnam, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

HANOI - Rais Xi Jinping wa China Jumanne alipokutana na wajumbe wa Mkutano wa Urafiki kati ya Watu wa China na Vietnam mjini Hanoi, Vietnam, akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam na Rais wa Vietnam Luong Cuong, amesema kwamba uhusiano kati ya China na Vietnam umekita mizizi kwa watu, kudumishwa na watu na kuwezeshwa na watu.

Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema, katika miaka mingi iliyopita, watu wa China na Vietnam wamesimama pamoja katika hali ngumu na nyepesi, kusaidiana katika shida na dhiki, na kwa pamoja wameandika ukurasa tukufu katika historia ya urafiki kati ya China na Vietnam.

Amesisitiza kuwa, urafiki kati ya China na Vietnam umekita mizizi na kukua kupitia kuungana mkono kati ya watu wa pande hizo mbili, na umechanua na kuzaa matunda kwa mshikamano na uratibu wao.

"Zikiwa zimedhamiria kufikia malengo makuu yenye sifa ya "mambo sita zaidi," yaani, kuaminiana zaidi kisiasa, ushirikiano mkubwa zaidi wa kiusalama, ushirikiano wa kina wa kivitendo, msingi imara wa imani ya watu, uratibu na ushirikiano wa karibu zaidi katika masuala ya pande nyingi, na usimamizi na utatuzi bora wa migongano, nchi hizo mbili zinaungana mkono kithabiti katika kufuata njia ya ujamaa inayolingana na hali halisi ya kila nchi, na kuendelea kupiga hatua mpya katika maendeleo ya mambo ya ujamaa,” amesema.

Rais Xi amesema,Watu ndiyo watengenezaji historia, kukubaliwa na kuungwa mkono wa watu wa pande hizo mbili kumeweka msingi imara wa kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja.

Amedhihirisha kuwa vijana ndiyo mustakabali na matumaini ya mambo ya vijana ya Vietnam, Rais Xi amesema kuwa katika miaka mitatu ijayo, China itawaalika vijana wa Vietnam kuja China kufanya "Ziara ya Mafunzo ya Vyama." (Red Study Tours)

Kwa upande wake, To Lam amesema, kufanyika kwa Mkutano wa Urafiki kati ya Watu wa China na Vietnam kuna umuhimu mkubwa katika wakati wa ziara hiyo ya kihistoria ya Rais Xi nchini Vietnam, maadhimisho ya kutimia miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, na Mwaka wa Mawasiliano kati ya Watu wa China na Vietnam.

To Lam amesema kuwa ushirikiano wa kirafiki siku zote umekuwa sehemu kuu ya uhusiano kati ya China na Vietnam, upande wa Vietnam daima utakumbuka kwamba chama cha CPC, serikali ya China na watu wa China wametoa msaada wa kujitolea kwa mchakato wa uhuru, muungano na maendeleo wa Vietnam.

Kabla ya shughuli hiyo, Rais Xi, akiambatana na To Lam na Luong Cuong, ametembelea kwenye maonyesho ya picha ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Vietnam.

Baadaye, viongozi hao kwa pamoja wamezindua mradi wa "Ziara ya Mafunzo ya Vyama." (Red Study Tours)

Rais Xi, To Lam na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh, kwa pamoja walishuhudia hafla ya uzinduzi wa mfumo wa ushirikiano wa reli kati ya China na Vietnam. 

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),  akiambatana  na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam na Rais wa Vietnam, Luong Cuong,  ametembelea kwenye maonyesho ya picha ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Vietnam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam na Waziri Mkuu wa Vietnam, Pham Minh Chinh, kwa pamoja wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa  mfumo wa ushirikiano wa reli kati ya China na Vietnam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano mjini Hanoi,Vietnam, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam na Waziri Mkuu wa Vietnam, Pham Minh Chinh, kwa pamoja wakishuhudia hafla ya uzinduzi wa  mfumo wa ushirikiano wa reli kati ya China na Vietnam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam na Rais wa Vietnam, Luong Cuong, kwa pamoja wakizindua mradi wa "Ziara ya Mafunzo ya Vyama" (Red Study Tours) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akitoa hotuba kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 15, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha