Afrika Kusini yaahidi jitihada zaidi kuanuwaisha maeno ya kuuza bidhaa na huduma nje

(CRI Online) April 15, 2025

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema serikali inaongeza juhudi za kuanuwaisha maeneo ya kuuza bidhaa na huduma za nchi hiyo nje ya nchi.

Mapema mwezi huu Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza sera ya kuongeza ushuru kwa makumi ya washirika wa kibiashara, ikiwa ni pamoja na ushuru wa asilimia 31 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Afrika Kusini lakini baadaye alisimamisha kuanza kutozwa ushuru huo kwa siku 90.

Rais Ramaphosa amesema biashara ya kimataifa ni sehemu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kwamba Afrika Kusini inaimarisha uhusiano na nchi na maeneo ambayo ina mikataba ya kikanda na ya kibiashara nazo, yakiwemo ya Umoja wa Forodha wa Kusini mwa Afrika, Eneo la Biashara Huria la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, na Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika.

Amesema Afrika Kusini itaendelea kutetea kuwepo kwa mazingira yenye haki na usawa kwa biashara ya kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha