Hamas yasema inapitia pendekezo jipya la amani ya Gaza kutoka kwa wapatanishi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 15, 2025

Wafanyakazi wa ulinzi wa raia wakimhamisha mwathiriwa kutoka kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa baada ya shambulizi la anga la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 13, 2025. (Picha na Mahmoud Zaki/Xinhua)

GAZA - Hamas imesema kwamba uongozi wake unapitia pendekezo la amani ya Gaza lililopokelewa kutoka kwa wapatanishi na itawasilisha majibu yake baada ya kukamilisha majadiliano ya ndani.

Katika taarifa yake ya Jumatatu jioni, Hamas imesema uongozi wake unachunguza pendekezo hilo "kwa wajibu mkubwa wa kitaifa" na itawasilisha majibu yake "mara tu majadiliano muhimu yatakapokamilika."

Kundi hilo limesisitiza matakwa yake ya msingi kwa makubaliano yoyote wezekana: "usimamishaji mapigano wa kudumu, kuondolewa kabisa kwa vikosi vya uvamizi kutoka Ukanda wa Gaza, mabadilishano ya kweli ya wafungwa, kuanza kwa mchakato makini wa ukarabati, na kuondoa mzingiro usio wa haki dhidi ya watu wetu huko Gaza."

Hamas haikutoa maelezo halisi ya pendekezo hilo katika taarifa hiyo.

Wapalestina takriban 1,613 wameuawa na wengine 4,233 kujeruhiwa tangu Israel iliporejelea mashambulizi yake makali Machi 18 katika Ukanda wa Gaza, mamlaka ya afya yenye makao yake mjini Gaza imesema Jumatatu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha