

Lugha Nyingine
SADC yakanusha madai ya operesheni za pamoja za kijeshi na vikosi vya DRC
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imekanusha madai kwamba kikosi chake cha kikanda kilichotumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kinaendesha operesheni za kijeshi za pamoja na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika taarifa iliyotolewa mjini Gaborone, makao makuu ya SADC jana Jumatatau, Jumuiya hiyo imekanusha madai yaliyotolewa na kundi la M23 katika taarifa ya tarehe 12 Aprili, ikiyaelezea kuwa si sahihi na ya kupotosha.
SADC imesema kwa sasa inatekeleza muundo na uratibu wa uondoaji kikosi chake kutoka DRC kwa mujibu wa maagizo kutoka mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC.
SADC pia imesisitiza kufuata matokeo ya mkutano wa mashauriano uliofanyika Machi 28, mjini Goma, kati ya wawakilishi wa SADC na uongozi wa kundi la M23.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma