

Lugha Nyingine
Mji wa Heze Mashariki mwa China Tayari Kutoa Uhondo wa Maua ya Majira ya Mchipuko
Kongamano la Dunia la Maua ya Peoni 2025 vilevile na Tamasha la 34 la Utalii wa Kitamaduni wa Maua ya Peoni, vimefunguliwa katika mji wa Heze, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Aprili 8.
Katikati ya mchanuo kamili wa maua ya peoni, Bustani ya Maua ya Peoni ya Caozhou inashuhudia maua ya kuvutia ya peoni yakiamka yakiwa na hamasa kubwa ya uhai, ikivutia watalii wengi kutoka maeneo ya mbali na karibu
Watalii wengi kutoka nje ya nchi wamesifu shughuli mbalimbali kwenye bustani hiyo mwaka huu, vilevile kazi ya ya maua ya peoni katika kukuza uchumi wa kienyeji.
Kwa mujibu wa takwimu, tasnia ya maua ya peoni katika mji huo wa Heze imetengeneza ajira takriban 500,000 na kuzalisha mapato yenye thamani ya jumla ya karibu yuan bilioni 13 (sawa na dola za Marekani bilioni 1.78)
Huku wimbi la Majira ya Mchipuko likitapakaa angani, mji wa Heze, unaojulikana kama "mji mkuu wa maua ya peoni wa China" uko tayari kuikaribisha dunia kwa uhondo wa maua.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma