

Lugha Nyingine
Xi azihimiza China na Vietnam kwa pamoja kusonga mbele kuelekea mambo ya kisasa
Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa China na Vietnam kusonga mbele kuelekea mambo ya kisasa bega kwa bega.
Kwenye mkutano wake jana Jumatatu na Mwenyekiti wa Bunge la Vietnam Tran Thanh Man, Rais Xi pia amehimiza pande hizo mbili kuchangia utulivu na nguvu chanya duniani, akisema kuwa nchi hizo mbili ziko katika kipindi muhimu cha kujitafutia maendeleo na kuelekea ustawishaji wa kitaifa.
Rais Xi amesema, katika hali ya kimataifa yenye mabadiliko na misukosuko, China na Vietnam zinapaswa kushikilia kithabiti kujiamini kuhusu njia na mifumo yao, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuendelea kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja inayobeba umuhimu wa kimkakati na kufanya kazi pamoja kuelekea mambo ya kisasa, zikiingiza utulivu na nguvu chanya zaidi duniani.
Kwa upande Tran Thanh Man amesema Vietnam na China, zinazopakana kwa milima na mito, zimejenga uhusiano mzuri wa dhati unaojumuisha "ukomredi pamoja na undugu" chini ya malezi ya uangalifu ya viongozi wa vyama na nchi hizo mbili, na uhusiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili umekuwa mzuri kwa muda mrefu.
Amesema ziara hiyo ya Rais Xi inadhihirisha kikamilifu umuhimu uliowekwa na Chama cha Kikomunisti cha China, nchi hiyo na watu wa China kwa uhusiano wa Vietnam na China.
Ameongeza kuwa makatibu wakuu wawili wa nchi hizo mbili wametoa mwongozo muhimu wa kimkakati katika kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya Vietnam na China yenye mustakabali wa pamoja inayobeba umuhimu wa kimkakati, hatua ambayo itafungua ukurasa mpya wa uhusiano wa pande mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma