Rais Xi atoa wito kwa China na Vietnam kupinga umwamba, maamuzi ya upande mmoja na kujilinda kibiashara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 15, 2025

Rais wa China Xi Jinping  ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

HANOI - Rais Xi Jinping wa China Jumatatu kwenye mkutano na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh, amezihimiza China na Vietnam kwa pamoja kupinga umwamba, maamuzi ya upande mmoja na kujilinda kibiashara.

Rais Xi amesema chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) na serikali ya Vietnam, nchi hiyo imepata utulivu wa kisiasa na kijamii, na kupata mafanikio ya kuvutia katika mageuzi, huku hadhi yake ya kimataifa ikiongezeka, hali ambayo inaifurahisha China.

"Pande zote mbili zinabeba wajibu wa dhamira ya kihistoria ya kufikia ustawishaji wa kitaifa na kuharakisha maendeleo ya kitaifa," Rais Xi amebainisha.

Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kujenga hisia ya jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na kuzidisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, ili kutumikia michakato yao ya ujenzi wa mambo ya kisasa, na kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema pande hizo mbili, zinapaswa kuimarisha uratibu wa kimkakati na kuimarisha msingi wa kisiasa kwa ajili ya kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja.

Amehimiza pande hizo mbili kuzidisha mabadilishano ya ngazi ya juu, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, na kwa pamoja kupinga umwamba, maamuzi ya upande mmoja na kujilinda kibiashara.

Rais Xi pia ametoa wito kwa pande hizo mbili kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, ili kwa pamoja kulinda haki na usawa wa kimataifa, na kulinda amani, utulivu, maendeleo na ustawi barani Asia na kwingineko.

Amesema China na Vietnam zinapaswa kutoa kutumika kikamilifu kwa faida zao za kijiografia za kuwa zimeunganishwa na ardhi na bahari, kuimarisha kuwiana kwa mikakati ya maendeleo na kutumia kikamilifu fursa za uwezekano wa ushirikiano wa kiviwanda.

Bw. Pham Minh Chinh amesema ziara ya Rais Xi nchini Vietnam ni mabadlishano muhimu zaidi ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili kwa mwaka huu, akiongeza kuwa hilo ni tukio kubwa na la furaha katika uhusiano wa Vietnam na China na lenye umuhimu wa kihistoria, na bila shaka litafanya uhusiano wa Vietnam na China kuwa na maendeleo makubwa zaidi na kuingiza msukumo mkubwa katika ushirikiano wa pande mbili.

Amesema nchi yake pia inatarajia kuimarisha ushirikiano na China katika masuala ya kimataifa na kikanda, ili kudumisha umakini wa kimkakati katika hali ngumu na tete ya kimataifa, na kwa pamoja kulinda ushirikiano wa pande nyingi na utaratibu wa kimataifa.

Rais Xi Jinping,wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha