Rais Xi Jinping atoa wito wa kuzidisha ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 15, 2025

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na katibu mkuu Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam,, kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya CPV mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na katibu mkuu Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam, kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya CPV mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

HANOI - Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye yuko kwenye ziara ya kiserikali nchini Vietnam, Jumatatu alipokutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam ametoa wito wa kuzidishwa kwa ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi amesema amefurahi kufanya ziara nchini Vietnam na kutimiza duru ya kwanza ya ziara za kutembeleana na Katibu Mkuu To Lam.

Mwaka huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa CPV, kumbukumbu ya miaka 80 ya kuanzishwa kwa Vietnam na maadhimisho ya miaka 50 tangu ukombozi wa eneo la Kusini la Vietnam, amesema anatoa pongezi nyingi kwa Vietnam kwa niaba ya CPC na serikali ya China.

Rais Xi pia amesema China kama ilivyofanya nyakati zote, itaiunga mkono Vietnam katika kufuata njia ya ujamaa inayoendana na mazingira yake ya taifa, kufanya kwa mafanikio Mkutano Mkuu wa 14 wa CPV mwaka 2026, na kuunga mkono juhudi zake thabiti za kufikia malengo mawili yaliyowekwa ya miaka mia moja ya chama na nchi.

“Zikikabiliana na dunia inayobadilika na yenye misukosuko, China na Vietnam zimeendelea kuwa na dhamira ya kujipatia maendeleo kwa amani na kuzidisha ushirikiano wao wa kirafiki, zikileta utulivu na uhakika unaohitajika sana duniani,” Xi amesema.

Zikiwa zimesimama katika mwanzo mpya kihistoria, pande hizo mbili zinapaswa kutumia mafanikio yaliyopita, kusonga mbele pamoja na kuhimiza urafiki mkubwa wa jadi unaojumuisha "urafiki na undugu," Xi amesema.

Rais Xi amependekeza hatua sita za kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja; ikiwa ni pamoja na kuongeza kuaminiana kimkakati katika ngazi ya juu zaidi, kujenga wigo imara zaidi wa usalama, kupanua ushirikiano wa kiwango cha juu wa kunufaishana, kuimarisha uhusiano wa kati ya watu wao, kufanya uratibu wa karibu wa pande nyingi, na kufikia mawasiliano chanya kuhusu mambo ya bahari.

To Lam amekaribisha ziara ya kiserikali ya Rais Xi nchini Vietnam, ambayo imefanyika wakati wa maadhimisho ya kutimia miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Amesema Rais Xi si tu ni kiongozi bora wa watu wa China bali pia ni rafiki mkubwa wa watu wa Vietnam.

Rais Xi Jinping wa China, amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam, kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya CPV mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China, akifanya mazungumzo na katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam,, kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya CPV mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China, akifanya mazungumzo na katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam, kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya CPV mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam, akimwalika Rais Xi Jinping, kwenye mazungumzo mafupi kabla ya mazungumzo yao rasmi kwenye makao makuu ya Kamati Kuu ya CPV mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China, na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) To Lam, wakiangalia nyaraka 45 za ushirikiano wa pande mbili zilizosainiwa na pande hizo mbili baada ya mazungumzo yao rasmi mjini Hanoi, Vietnam, Aprili 14, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha