

Lugha Nyingine
Mradi wa bwawa kubwa la Ethiopia wakamilika kwa 98.66%
Mradi wa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) umekamilika kwa asilimia 98.66, na mitambo sita ya kuzalisha umeme imeanza kufanya kazi.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Fana, mchakato wa maendeleo ulitangazwa wakati serikali ya Ethiopia ilipoanza kikao chake cha miezi tisa cha kukagua utendaji kazi kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 wa Ethiopia ulioanzia Julai 8, 2024.
Maofisa wamebainisha kuwa bwawa hilo linakaribia kukamilika na linachukua jukumu muhimu katika kupanua uzalishaji wa umeme nchini Ethiopia na usambazaji wa umeme wa kikanda.
Kwenye kikao cha bunge kilichofanyika mwezi uliopita, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema bwawa hilo litazinduliwa ndani ya miezi sita, akilitaja kama ishara ya kujitegemea na juhudi za pamoja huku kukiwa na shinikizo la kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma