

Lugha Nyingine
Tanzania yazindua kiwanda cha kwanza cha kuzalisha baruti na vilipuzi ili kusaidia sekta ya madini
Waziri wa Madini wa Tanzania Bw. Anthony Mavunde amezindua kiwanda cha kwanza cha kuzalisha baruti na vilipuzi nchini humo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza uongezaji thamani na kusaidia ukuaji wa viwanda vinavyohudumia sekta za kimkakati kama ya madini.
Bw. Mavunde amesema kuzinduliwa kwa kampuni ya Solar Nitrochemicals iliyopo wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, kutaimarisha kwa kiasi kikubwa shughuli za uchimbaji madini nchini humo.
Amesisitiza dhamira ya serikali ya kuweka mazingira salama na mazuri kwa wawekezaji, na kutoa mchango wao katika kuongeza mapato na ajira kwa Watanzania. Mahitaji ya Tanzania ya baruti kwa mwaka ni tani elfu 26 na vipande milioni 10.
Kiwanda hicho kipya kinatarajiwa kuzalisha tani elfu 22 za baruti na vipande milioni 15 vya vilipuzi kila mwaka, uwezo unaotarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji kutoka nje na kuongeza mauzo ya nje kwa nchi jirani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma