“Miaka 50 ya Kikundi cha madaktari wa China kutoa huduma nchini Niger”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2025

Picha inaonyesha madaktari wa kikundi cha 21 cha madaktari wa China waliopelekwa nchini Niger na daktari mwenyeji wakimchunguza mgonjwa katika Hospitali Kuu ya Niger mjini Niamey, tarehe 7 Agosti 2019. (Xinhua)

Picha inaonyesha madaktari wa kikundi cha 21 cha madaktari wa China waliopelekwa nchini Niger na daktari mwenyeji wakimchunguza mgonjwa katika Hospitali Kuu ya Niger mjini Niamey, tarehe 7 Agosti 2019. (Xinhua)

Miaka mitatu iliyopita, Hama Moctar aliyekuwa na umri wa miaka mitano alivunjika vibaya mguu wake wa kushoto. Baadaye alipata maambukizo, na mguu wake ukawa mfupi kwa sentimita 10. Madaktari wenyeji walisisitiza kukata mguu ndio njia pekee. Nong Jianbu, daktari wa majeraha kutoka kikundi cha 24 cha madaktari wa China nchini Niger, alipendekeza mbinu mbadala, yaani mbinu ya Ilizarov.

Kwa kutumia mashine kutoka China na juhudi za pamoja, madaktari wa China na Niger walimfanyia Moctar upasuaji ngumu. Kwa sasa, miguu yote ya Moctar ina urefu sawa na anaweza kutembea tena kwa uhuru.

Hospitali ya rufaa iliyojengwa na China mwezi Agosti, mwaka 2016 ni moja ya vituo vikubwa vya matibabu katika eneo la Afrika Magharibi. Ni alama ya uhusiano wa pande mbili uliopo kwa zaidi ya nusu karne.

Tangu 1976, vikundi vya madaktari wa China kutoka Mkoa wa Guangxi vimefanya kazi kwa bidii nchini Niger, na kutoa mchango mkubwa katika mfumo wa afya wa nchi hiyo.

Tangu mwaka 1976, madaktari zaidi ya 750 wa China wamewatibu karibu wagonjwa milioni 1 nchini Niger. “Kila mgonjwa aliyepona anaandika ukurasa mpya katika historia ya urafiki kati ya China na Afrika.” alisema Zheng Zhida, mkuu wa kikundi cha 24 cha madaktari wa China.

"Ushirikiano wetu na China umekuwa na matokeo mengi," alisema Mamane Daou, mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, akiongeza kuwa si kama tu kikundi cha madaktari wa China kimetuma madaktari wenye ujuzi, bali pia kimetoa mashine na vifaa muhimu vya matibabu.

"Ujuzi na juhudi zao vimetufanya tuwaheshimu sana," alisisitiza. "Hospitali hii sasa inapokea wagonjwa hata kutoka Mali na Burkina Faso."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha