

Lugha Nyingine
China yasema iko tayari kuendeleza miradi ya reli ya SGR na Vietnam
(CRI Online) April 14, 2025
Rais Xi Jinping wa China amesema China iko tayari kuendeleza ushirikiano na Vietnam kwenye reli tatu za kiwango cha SGR kaskazini mwa Vietnam na bandari ya kisasa.
Rais Xi amesema hayo katika makala iliyochapishwa na Gazeti la Nhan Dan la Vietnam Siku chache kabla ya ziara yake nchini humo. Kwenye makala hiyo Rais Xi pia amesema China na Vietnam zinapaswa kuimarisha ushirikiano kwenye mambo ya viwanda na ugavi, na kupanua ushirikiano katika sekta zinazoibukia kama vile mtandao wa 5G, akili bandia na maendeleo ya kijani.
Rais Xi pia amesema China itazidisha ushirikiano wa kirafiki na nchi jirani na kuendeleza kwa pamoja Asia kuwa ya kisasa. Ameongeza kuwa China itahakikisha uendelevu na utulivu wa diplomasia na majirani zake.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma