

Lugha Nyingine
Wizara ya Biashara ya China Yajibu Kuhusu Marekani kutotoza “Ushuru wa Reciprocal” kwa Baadhi ya Bidhaa
Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China tarehe 13 alisema, tarehe 12 Aprili kwa saa za Mashariki ya Marekani, upande wa Marekani ulitangaza waraka wa kumbukumbu husika za kutotoza “ushuru wa reciprocal” kwa baadhi ya bidhaa zikiwemo kompyuta, simu janja, vifaa vya kutengeneza semikonda na vifaa vya IC. Kwa sasa, China inafanya tathmini juu ya athari za hatua hiyo.
Msemaji huyo alisema, “Tumefuatilia kuwa haya ni marekebisho ya pili ya sera husika yaliyofanywa na Marekani baada ya kuahirisha kutoza ushuru mkubwa wa ‘Reciprocal’ kwa baadhi ya wenzi wake wa kibiashara tarehe 10 Aprili. Hii ni hatua ndogo kwa Marekani kurekebisha sera yake potofu ya ‘ushuru wa Reciprocal’ uliotozwa wa upande mmoja.”
Alibainisha kuwa kutoa ushuru wa Reciprocal kwa kutumia agizo la kiutawala si tu kunakiuka kanuni za msingi za kiuchumi na soko, bali pia kunapuuzia ushirikiano wa kunufanishana na uhusiano wa utoaji na uhitaji kati ya nchi na nchi. Tangu ushuru huu utangazwe Aprili 2, haujatatua matatizo yoyote ya Marekani, bali umeharibu kwa kiasi kikubwa utaratibu wa uchumi na biashara ya kimataifa, kuathiri uzalishaji na uendeshaji wa kawaida wa makampuni, na matumizi ya kila siku ya watu, hivyo huleta madhara kwa wengine bali pia kwao wenyewe.
Msemaji huyo alisisitiza kuwa msimamo wa China kuhusu uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani umekuwa thabiti: vita vya kibiashara havina mshindi, na kujilinda kibiashara si suluhisho. Usemi wa kale wa China unasema, “Anayeweza kufungua kengele ndiye aliyeifunga.” Tunahimiza upande wa Marekani kuzingatia sauti za kimantiki kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na pande zote za ndani ya nchi, kuchukua hatua kubwa ya kurekebisha makosa, kufuta kabisa hatua potofu ya “ushuru wa Reciprocal”, na kurejea katika njia sahihi ya kuheshimiana na kutatua tofauti kwa mazungumzo ya usawa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma