Rais wa China awasili Vietnam na kuanzia ziara rasmi nchini humo

(CRI Online) April 14, 2025

Rais Xi Jinping wa China amewasili nchini Vietnam na kuanza ziara rasmi nchini humo.

Kwenye hotuba yake aliyotoa kwenye uwanja wa ndege mjini Hanoi, rais Xi amesema huu ni mwaka wa 75 tangu China na Vietnam kuanzisha uhusiano wa kibalozi. Katika mwanzo mpya, China inapenda kushirikiana na Vietnam kwa kiwango cha juu zaidi, katika nyanja nyingi zaidi, na kwa kina zaidi, ili kunufaisha watu wa nchi hizo mbili na dunia nzima.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha