

Lugha Nyingine
Baraza la Djibouti lahimiza ushirikiano kuimarishwa huku kukiwa na misukosuko ya sera duniani
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed akizungumza kwenye hafla ua ufunguzi wa Mkutano wa pili wa Baraza la Djibouti, Djibouti City, mji mkuu wa Djibouti, Aprili 7, 2025. (Xinhua/Habtamu Worku)
DJIBOUTI CITY – Wakikiri kuongezeka kwa misukosuko inayosababishwa na sera duniani, viongozi wa biashara na watunga sera katika Baraza la Djibouti wametoa wito wa kujenga upya matumaini na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja.
Wito huo umetolewa wakati viongozi 150 wa biashara na watunga sera kutoka nchi 51 wakikusanyika katika Baraza la Pili la Djibouti, shughuli kubwa ya biashara ya kimataifa ambalo linalenga kushirikisha wawekezaji binafsi na wa kitaasisi ili kulifanyia mageuzi taifa hilo la Bahari Nyekundu na Bara zima la Afrika.
Likifanyika chini ya kaulimbi ya "Kufungua Fursa za Ukuaji wa Kikanda na wa Dunia" katika Djibouti City kuanzia Jumapili hadi Jumanne wiki hii, Baraza hilo limesema kuwa misukosuko hiyo ya hivi karibuni duniani, mingi yao yanasababishwa wenyewe, inatumika kama kengele kwa ajili ya kuamsha nchi za Afrika na kwingineko kujenga ubia wa kimkakati na uhamasishaji wa rasilimali za ndani.
Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi, Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed amesisitiza uchumi wenye anuai ni suluhisho mwafaka katika kukabiliana na hali ya sintofahamu duniani.
Amesema katika Dunia inayobadilika kwa kasi, ambapo uhakika wa jana hauwezi kuhakikishwa tena, Djibouti inajitahidi kudumisha utulivu wake na kubadilika kuendena na mabadiliko.
Waziri Mkuu huyo amezungumzia juhudi za nchi hiyo katika kuanuaisha uchumi wake zaidi ya sekta yake iliyoimarishwa vizuri ya bandari na uchukuzi, huku ikifanya uwekezaji katika nishati mbadala, uchumi wa kidijitali, utalii, na huduma za mambo ya fedha.
Carlos Lopes, katibu mtendaji wa zamani wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi kwa Afrika (UNECA) na ambaye kwa sasa ni profesa wa heshima katika Shule ya Mandela ya Utawala wa Umma katika Chuo Kikuu cha Cape Town, ameelezea wasiwasi wake juu ya hali ya sasa ya kutokuwa na uhakika kwenye siasa za kijiografia na kuongezeka kwa kujihami kiuchumi, ambayo inaleta changamoto kubwa kwa uchumi wa Afrika.
Amesema kuwa uchumi wa Afrika umeathiriwa vibaya na mmomonyoko wa hivi karibuni "ambao haujatokea hapo awali" wa mfumo wa pande nyingi, uliosababishwa na msururu wa misukosuko inayotokana na janga la COVID-19 na mgogoro nchini Ukraine.
Baraza hilo limeshirikisha wazungumzaji mashuhuri zaidi ya 50, wakishiriki katika mijadala inayohusu mada kama vile ubinafsishaji, ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, na sekta muhimu za kiuchumi kama vile teknolojia, muunganisho, nishati, utalii, huduma za mambo ya fedha na usambazaji bidhaa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma