Nigeria yasisitiza dhamira ya kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing

(CRI Online) April 11, 2025

Serikali ya Nigeria imesisitiza dhamira yake ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwaka jana mjini Beijing, ikisisitiza kusudi lake la kutumia ushirikiano huo kuhimiza maendeleo endelevu.

Mkurugenzi wa Idara ya Kanda katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria, Bi. Janet Olisa ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa uzinduzi wa kamati ya ngazi ya juu ya kati ya wizara uliofanyika Jumatano mjini Abuja.

Kamati hiyo imepewa jukumu la kufanya makubaliano mbalimbali yaliyosainiwa katika mkutano wa FOFAC na kwenye ziara ya Rais wa Nigeria Bola Tinubu nchini China kuwa miradi halisi ya maendeleo itakayoleta manufaa kwa nchi hiyo.

Bi. Olisa, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo, amebainisha kuwa utekelezaji utaangazia kuendeleza vipaumbele vya Nigeria katika sekta muhimu zikiwemo za kilimo, uchumi wa kidijitali na maendeleo ya miundombinu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha