Ethiopia kuandaa walimu wenyeji wa lugha ya Kichina katika Jimbo la Oromia

(CRI Online) April 11, 2025

Chuo Kikuu cha Addis Ababa na Idara ya Elimu ya Jimbo la Oromia nchini Ethiopia wamekubaliana kutoa mafunzo ya kuandaa walimu wenyeji wa lugha ya Kichina katika Jimbo la Oromia, ambalo ni kubwa zaidi nchini humo.

Pande hizo mbili zimesaini mkataba wa makubaliano (MoU) Jumatano wiki hii mjini Addis Ababa, kuhusu kutoa mafunzo kwa walimu hao katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, kuanzia mwaka ujao wa masomo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Addis Ababa Samuel Kifle, makubaliano hayo yanahusisha ujengaji uwezo wa walimu wa lugha ya Kichina katika shule za sekondari na za bweni jimboni Oromia, na yanalenga kutoa mafunzo kwa walimu wapatao 30 kila mwaka.

Bw. Samuel Kifle amesema, mpango huo unaendana na dhamira ya serikali ya shirikisho ya kupanua elimu ya lugha za kigeni, ikiwemo Kichina, kote nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha