Wafanyakazi wa afya nchini Sudan Kusini wajiunga na kozi ya lugha ya Kichina

(CRI Online) April 11, 2025

Kozi ya tano ya lugha ya Kichina kwa wafanyakazi wa afya nchini Sudan Kusini imeanza jana Alhamis, ikivutia wanafunzi zaidi ya 70 walio na shauku ya kujifunza na kutumia fursa za kupata ufahamu mzuri wa lugha ya Kichina.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa kozi hiyo, mkurugenzi wa miradi katika Wizara ya Afya nchini Sudan Kusini, Yousif Deng Riak Deng amehimiza wanafunzi hao kutumia fursa ya kujifunza lugha ya Kichina kwa kuwa inasadia kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Ameongeza kuwa, sekta ya afya ni eneo la kipaumbele kwa ushirikiano wa China na Sudan Kusini, ambao umepata matunda yaliyopelekea kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa China nchini Sudan Kusini Huo Ying amesema, lugha ya Kichina imekuwa maarufu sana duniani kutokana na mabadilishano mapana na ya kina na ushirikiano kati ya watu wa China na wa kimataifa.

Amesema lugha ya Kichina imesaidia vijana wa Sudan Kusini, hususan kwenye sekta ya afya, kuielewa vizuri China, pamoja na utamaduni na maendeleo yake, ikiwemo mchango wa China kwa amani ya dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha