

Lugha Nyingine
Rais wa Zambia ahimiza uwekezaji katika shoroba za usafirishaji ili kukuza biashara ya ndani ya Afrika
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametoa wito wa uwekezaji zaidi katika maendeleo ya miundombinu barani Afrika kwenye mkutano unaolenga kutatua changamoto zinazozikabili sekta za usafirishaji na uchukuzi barani uliofunguliwa Lusaka, Zambia jana Alhamisi.
Akihutubia Mkutano huo wa nne wa Muunganisho wa Nchi Kavu wa Zambia Rais Hichilema amesema kuboresha shoroba za usafirishaji kunaweza kukuza biashara ya ndani ya Afrika, ambayo sasa bado iko katika kiwango cha chini kutokana na matatizo yaliyopo ikiwemo mifumo isiyo toshelezi ya usafirishaji.
Ameeleza kuwa ni muhimu sana kuwekeza katika vituo vya huduma zote katika sehemu moja vya mipakani ili kurahisisha mtiririko wa biashara, na kuongeza kuwa, uwekezaji wa pamoja katika miundombinu wa nchi za Afrika utaleta matokeo mazuri zaidi kuliko ule wa nchi moja moja.
Ametoa wito kwa sekta binafsi kushirikiana na serikali kuunga mkono maendeleo ya miundombinu ili kupunguza gharama za kuendesha biashara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma