

Lugha Nyingine
Tovuti za Kivietinamu, Kiurdu na Kihindi zimeanzishwa kwenye Tovuti ya Gazeti la Umma
Ili kupanua maeneo ya kupata habari kutoka kwenye Tovuti ya Gazeti la Umma na kuwafikia wasomaji wengi zaidi, Tovuti ya Kivietinamu, Tovuti ya Kiurdu na Tovuti ya Kihindi zimeanzishwa rasmi kuanzia tarehe 11 kwenye Tovuti ya Gazeti la Umma.
Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ilitoa matakwa bayana kuwa, “kuimarisha ujenzi wa uwezo wa kufanya uenezi duniani, kuongeza kwa pande zote ufanisi wa uenezi duniani, ili kupata haki ya kutoa sauti duiani inayoendana na nguvu na nafasi za nchi yetu duniani. Kuimarisha mawasiliano ya ustaarabu na kufundishana, na kuhimiza utamaduni wa China uelekee duniani vizuri zaidi.” Kuanzishwa kwa Tovuti tatu mpya ndiyo hatua muhimu ya Tovuti ya Gazeti la Umma kwa kuimarisha ujenzi wa uwezo wa mawasiliano. Tovuti hizo tatu zitatoa habari za China za pande zote kwa watu wa maeneo husika, na kujenga zaidi mfumo wa mawasiliano ya kimataifa ya Tovuti ya Gazeti la Umma ili iwe “chombo cha habari kinachotumia lugha mbalimbali, chenye majukwaa mengi, chenye vyombo vya habari vya aina zote, na kinachoelekea utandawazi wa kimataifa”.
Katika miaka ya hivi karibuni, Tovuti ya Gazeti la Umma imeanzisha matoleo kadhaa ya lugha za kigeni, kwa sasa idadi ya matoleo yake mtandaoni imefikia lugha 18 ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kirusi, Kiarabu, Kihispania, Kijapan, Kikorea, Kijerumani, Kireno, Kiswahili, Kiitalia, Kikhazak (Kikiril), Kithai, Kimalay, Kigiriki, Kivietinamu, Kiurdu na Kihindi, ikiifanya kuwa moja ya vyombo muhimu vya habari vya kitaifa vyenye matoleo ya lugha za kigeni nyingi zaidi mtandaoni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma