Rais Xi Jinping atumia salamu ya pongezi kwa mkutano wa 9 wa CELAC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametumia salamu ya pongezi kwa mkutano wa 9 wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Latini Amerika na Karibiani (CELAC) uliofunguliwa Jumatano wiki hii huko Tegucigalpa, mji mkuu wa Honduras.

Kwenye salamu hiyo ya pongezi, Rais Xi amesema kwamba dunia leo inapitia mabadiliko ya kasi haijapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, na Nchi za Kusini, ikiwemo China na nchi za Latini Amerika na Karibiani, zinakua kwa mwelekeo wenye nguvu kubwa.

“Jumuiya ya CELAC siku zote inashikilia kujitawala, kujitegemea na kuwa na mshikamano na nguvu ya kustawisha, ikitoa mchango muhimu katika kulinda amani na utulivu wa kikanda, kuhimiza maendeleo na ushirikiano, na kuhimiza umoja wa kanda hiyo. ”amesema.

Rais huyo wa China amezitakia kwa dhati nchi na watu wa Latini Amerika na Karibiani mafanikio makubwa zaidi katika njia ya kuelekea maendeleo na ustawishaji ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya mshikamano na ushirikiano wa Nchi za Kusini.

Rais Xi amesema, Uhusiano wa China na Latini Amerika umestahimili majaribu ya msukosuko wa kimataifa na kuingia katika kipindi kipya cha usawa, kunufaishana, uvumbuzi, uwazi na manufaa halisi kwa watu.

“Pande hizo mbili zimezidisha kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano wa kivitendo na kuimarisha mawasiliano kati ya watu na watu, yakileta manufaa kwa watu wa pande zote mbili na kuweka mfano kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini,” na China inapenda kushirikiana na nchi katika eneo hilo ili kusukuma mbele maendeleo mapya katika kujenga jumuiya ya China na Latini Amerika yenye mustakabali wa pamoja.

“Mwaka huu, China itakuwa mwenyeji wa mkutano wa nne wa mawaziri wa Jukwaa la China-CELAC mjini Beijing,” Rais Xi amesema.

“Nchi zote wanachama wa CELAC zinakaribishwa kuungana na China katika juhudi za pamoja za kuwezesha maendeleo na ushirikiano na kuchangia hekima na nguvu katika kukabiliana na changamoto za kimataifa, kuchochea mageuzi katika usimamizi wa kimataifa na kulinda amani na utulivu wa dunia,” Rais Xi amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha