China yachukua hatua kali za kulipiza dhidi ya ukandamizaji wa ushuru wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2025

BEIJING - China imechukua hatua za haraka na thabiti za kulipiza kisasi kufuatia Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China hivi karibuni, ili kulinda haki na maslahi yake halali ambapo serikali ya China imetangaza jana Jumatano kwamba itaongeza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani hadi asilimia 84, kuongeza kampuni sita za Marekani kwenye orodha yake ya mashirika yasiyoaminika, na kuweka mashirika 12 ya Marekani kwenye orodha yake ya udhibiti wa mauzo ya nje.

Hatua hizo -- zote zikiwa zimepangwa kutekelezwa rasmi kuanzia saa 6:01 mchana leo Alhamisi – zimekuja baada ya China kuahidi kuchukua hatua za kulipiza kisasi kwa "nia thabiti" na "njia tele" kufuatia uamuzi wa Marekani kuongeza kile kinachoitwa ushuru wa Reciprocal kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China hadi asilimia 84 kutoka asilimia 34 ya awali.

China pia imefungua kesi dhidi ya Marekani kwenye utaratibu wa kutatua migogoro wa Shirika la Biashara Duniani kuhusu ongezeko hilo jipya la ushuru.

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China siku hiyohiyo imetoa waraka kufafanua uhalisia wa mambo kuhusu uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, na kufafanua msimamo wa China katika masuala husika.

"Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ni wa kunufaishana, na ushirikiano unanufaisha pande hizo mbili huku makabiliano yanadhuru pande zote mbili," umesema waraka huo.

Afisa wa Wizara ya Biashara ya China amesema katika taarifa yake ya Jumatano kwamba, hivi karibuni, Marekani imeanzisha raundi kadhaa za kuongeza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China, na China imejibu hatua hizo kwa hatua kali za kulipiza.

"Nataka kusisitiza kwamba hakuna mshindi katika vita vya kibiashara, na kwamba China haitaki vita vya kibiashara. Lakini serikali ya China kwa vyovyote vile haitakaa ikitazama tu wakati haki na maslahi halali ya watu wake yanaumizwa na kunyimwa," afisa huyo amesema.

Ameeleza kwamba Marekani inachukua ushuru kama silaha ya kuweka shinikizo la juu na kufuata maslahi yake binafsi ni kitendo cha kawaida cha uamuzi wa upande mmoja, kujihami na ukamdamizaji wa kiuchumi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha