Biashara ya nje ya China yaelezwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na hatari na changamoto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2025
Biashara ya nje ya China yaelezwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na hatari na changamoto
Picha hii ikionyesha magari yanayosubiri kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi katika Bandari ya Yantai, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Januari 2, 2025. (Picha na Tang Ke/Xinhua)

BEIJING - Biashara ya nje ya China ina imani na uwezo wa kukabiliana na hatari na changamoto mbalimbali, Xiao Lu, afisa wa Wizara ya Biashara ya China amesema Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing.

“Uwezo mkubwa wa soko la China unaonekana siku hadi siku, na hatua zinazolenga kutuliza uchumi na biashara ya nje zinatekelezwa hatua kwa hatua. Mwelekeo wa kimsingi wa maendeleo mazuri ya muda mrefu ya kiuchumi bado haujabadilika,” Xiao ameuambia mkutano huo na waandishi wa habari.

“Hata hivyo, uchumi wa dunia kwa sasa unakabiliwa na hali nzito isiyo na uhakika, hasa katika sekta ya biashara, ambapo utulivu wa minyororo ya usambazaji bidhaa unakabiliwa na tishio,” Xiao amesema.

Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) limeonya kwamba "vita vya biashara" vipana vinaweza kusababisha kuongezeka kwa vizuizi vya biashara. Kutokana na hayo, OECD imerekebisha makadirio yake ya ukuaji wa uchumi duniani mwaka 2025 kushuka chini kwa asilimia 0.2 hadi asilimia 3.1. Kinyume chake, imeongeza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa China kwa asilimia 0.1.

"Marekebisho haya yanaonyesha imani ya jumuiya ya kimataifa katika uchumi wa China na matumaini yake yanayoongezeka kuhusu matarajio ya maendeleo ya China," Xiao amesema.

Kwa mujibu wa takwimu za wizara hiyo, Mwaka 2024, uagizaji na uuzaji nje bidhaa wa China ulifikia yuan trilioni 43 (dola za Kimarekani karibu trilioni 5.97). Imekuwa mshirika mkuu wa kibiashara kwa nchi na maeneo zaidi ya 150 na imetia saini makubaliano 23 ya biashara huria na nchi na maeneo 30.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha