Rais Xi atoa wito wa kujenga jumuiya ya nchi jirani yenye mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2025

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kamati kuu ya Chama wa kazi zinazohusiana na nchi jirani uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), kwenye mkutano wa kamati kuu ya Chama wa kazi zinazohusiana na nchi jirani, uliofanyika Beijing kuanzia Jumanne hadi Jumatano wiki hii, ametoa wito wa kujenga jumuiya ya nchi jirani yenye mustakabali wa pamoja na kujitahidi kuanzisha hali mpya ya kazi za ujirani mwema za China.

Katika hotuba yake, Rais Xi amefanya majumuisho kuhusu mafanikio na uzoefu wa kazi za jumla kuhusu kazi za ujirani za China katika zama mpya, akichambua kisayansi hali ya hivi sasa, na kuainisha malengo, kazi, mawazo na hatua za kipindi kijacho kuhusu kazi za ujirani.

Wakati akiongoza mkutano huo, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesisitiza kutekeleza kwa umakini msingi wa hotuba hiyo muhimu ya Rais Xi na kutekeleza kwa vitendo halisi kazi mbalimbali zinazohusu nchi jirani.

Mkutano huo umesisitiza kuwa China ina eneo kubwa la ardhi na mipaka mirefu, kufanya ujirani mwema ni msingi muhimu wa kupata maendeleo na ustawi, ni kazi muhimu kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, ni kazi inayopewa kipaumbele katika mambo ya diplomasia ya jumla ya nchi, na ni kiungo muhimu katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Mkutano huo umesema, ni lazima kutendea mambo ya maeneo jirani kwa mtazamo wa kimataifa na kuimarisha hisia ya kubeba wajibu na kutekeleza majukumu kwa ajili ya kufanya vizuri kazi za ujirani za China.

Mkutano huo umesema kuwa baada ya Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, China imetoa wazo la upendo, udhati, kunufaishana na ujumuishaji kuhusu mambo ya diplomasia yake ya ujirani, kutetea kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya nchi jirani yenye mustakabali wa pamoja.

“Kwa kuongozwa na diplomasia ya mkuu wa nchi, China imezidisha ushirikiano wa pande zote na nchi jirani, kuimarisha mawasiliano katika sekta mbalimbali, kulinda amani na utulivu kwa pamoja, na kuhimiza kazi za ujirani kupata mafanikio ya kihistoria na mageuzi” mkutano huo umeeleza.

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kamati kuu ya Chama wa kazi zinazohusiana na nchi jirani uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha