

Lugha Nyingine
Namibia yaihimiza Marekani kufuata kanuni za WTO kufuatia uamuzi wa kutoza ushuru mpya
Namibia imetoa wito kwa Marekani kufuata kanuni za biashara za kimataifa na kuwasiliana kwa uwazi na nchi zilizoathiriwa kufuatia uamuzi wa Serikali ya Marekani wa kutoza ushuru mpya kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi za nje, ikiwemo Namibia.
Akiongea na wabunge wa nchi hiyo, Waziri wa Uhusiano ya Kimataifa na Biashara Selma Ashipala-Musavyi amesema Marekani ilichukua hatua ya upande mmoja ya kutangaza ushuru mpya kupitia amri tendaji namba 14257 Aprili 2 na kwamba sera hiyo ni pamoja na ushuru wa kutozana sawa wa asilimia 21 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa nchini humo kutoka Namibia, utakaoanza kufanya kazi leo Aprili 9.
Waziri huyo ameonya kuwa hatua za kibiashara za upande mmoja kama hizo zinaweza kukiuka kanuni za Shirika la Biashara Duniani (WTO), kuhujumu mfumo wa pande nyingi, na kuharibu nchi zenye uchumi mdogo kama Namibia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma