Benki kuu ya Kenya yapunguza riba ya mikopo ili kuongeza mikopo ya sekta binafsi

(CRI Online) April 09, 2025

Benki Kuu ya Kenya (CBK) imepunguza kiwango cha riba ya mikopo hadi asilimia 10 kutoka asilimia 10.75 ili kuongeza mikopo kwa sekta binafsi.

Kamau Thugge, Gavana wa CBK ambaye aliongoza kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) huko Nairobi, amesema kuwa kuna uwezekano wa kurahisisha zaidi msimamo wa sera ya fedha ili kuchochea ukopeshaji wa benki kwa sekta binafsi na kuunga mkono shughuli za kiuchumi huku kukiwa na kuhakikisha utulivu wa kiwango cha ubadilishaji fedha.

Katika taarifa iliyotolewa Nairobi jana Jumanne, Thugge amesema wastani wa viwango vya mikopo umekuwa ukipungua polepole tangu Desemba 2024, lakini ukuaji wa mikopo ya sekta binafsi bado umeendelea kuwa chini.

Gavana huyo wa CBK ameongeza kuwa kamati ilikutana kutokana na kuongezeka kwa sintofahamu kwenye mtazamo wa kimataifa kuhusu ukuaji, mfumuko wa bei ambao unapungua lakini bado utadumu katika nchi zenye uchumi mkubwa, kuongezeka kwa mvutano wa kibiashara, na mivutano inayoendelea ya siasa za kijiografia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha