

Lugha Nyingine
Wataalamu wa kimataifa watoa wito wa ushirikiano wa kisayansi wa Kusini na Kusini ili kuimarisha usalama wa chakula
Xu Xun (kulia), mkurugenzi wa BGI-Research, akizungumza kwenye mkutano katika Wiki ya Sayansi ya Kikundi cha Mashauriano juu ya Utafiti wa Kimataifa wa Kilimo (CGIAR) jijini Nairobi, Kenya, Aprili 8, 2025. (Xinhua/Han Xu)
NAIROBI - Kampuni kubwa ya China ya jenomiki ya Kundi la BGI imesisitiza dhamira yake kwa ushirikiano wa Kusini na Kusini katika utafiti na kuendeleza aina bora za mpunga ili kukabiliana na tatizo la njaa na utapiamlo barani Afrika, watendaji wakuu na watafiti wamesema.
Wang Jian, mwanzilishi mwenza na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kundi la BGI, amesisitiza siku ya Jumatatu kuwa ushirikiano kati ya nchi za Kusini ambazo zina bioanuwai ni muhimu katika kuendeleza aina za mpunga zenye mavuno mengi na kuimarisha usalama wa chakula katika bara zima.
Akizungumza kwenye shughuli ya pembezoni mwa Wiki ya Sayansi ya Kikundi cha Mashauriano juu ya Utafiti wa Kimataifa wa Kilimo (CGIAR) jijini Nairobi, Kenya, Wang amezungumzia ushirikiano unaoendelea wa BGI na taasisi za Afrika katika kuendeleza na kueneza mpunga wa kuishi maisha marefu.
Xu Xun, mkurugenzi wa taasisis ya utafiti wa BGI amesema kuwa mpunga wa kuishi maisha marefu unastahimili hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na ukuaji wa miji. Amesema, zao hilo, ambalo linaweza kuvunwa kwa misimu mingi bila kupandwa tena, lilitajwa kuwa mojawapo ya mafanikio 10 ya juu ya kisayansi ya 2022 na jarida la Science.
Kama sehemu ya juhudi zake pana, BGI inafanya kazi na Muungano wa Mazao ya Yatima wa Afrika, unaoungwa mkono na Umoja wa Afrika, kufungua siri za kinasaba za mazao 101 ya jadi ya Afrika, Xu ameeleza.
Wang amesema kuwa taasisi za China zinapenda kuzidisha ushirikiano na washirika wa Afrika katika utafiti, mafunzo, na uhamishaji teknolojia ili kuendeleza aina mpya za mpunga chotara na kukidhi mahitaji ya lishe ya idadi ya watu inayoongezeka barani Afrika.
Ukiwa umetengenezwa kwa kuanzisha jeni kutoka kwenye spishi za mpunga wa mwituni kuwa aina za kawaida, mpunga huo wa maisha marefu tayari umeshaanzishwa nchini Uganda, Rwanda, na Madagascar.
Apollinaire Djikeng, mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo yenye makao yake makuu mjini Nairobi, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Kusini na Kusini katika sayansi, utafiti, uvumbuzi, na uhamisho wa teknolojia.
Wawakilishi wa Kundi la BGI na wadau wa jumuiya ya wanataaluma na wataalam duniani wakihudhuria mkutano katika Wiki ya Sayansi ya Kikundi cha Mashauriano juu ya Utafiti wa Kimataifa wa Kilimo (CGIAR) jijini Nairobi, Kenya, Aprili 8, 2025. (Xinhua/Han Xu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma