Hisa za Marekani zashuka baada ya hali ya kutokuwa na uhakika na ushuru kurejea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2025

Mfanyabiashara akifanya kazi katika soko la hisa la New York, mjini New York, Marekani, Aprili 8, 2025. (picha na Michael Nagle/Xinhua)

Mfanyabiashara akifanya kazi katika soko la hisa la New York, mjini New York, Marekani, Aprili 8, 2025. (picha na Michael Nagle/Xinhua)

NEW YORK – Soko la Hisa za Marekani limefunga kwa kushuka chini kwa kasi jana Jumanne, baada ya Ikulu ya White House kuthibitisha mipango ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China ambapo Wastani wa Kiviwanda wa Soko la Dow Jones ulipungua pointi 320.01, au asilimia 0.84, kufungwa katika 37,645.59, S&P 500 ilishuka kwa asilimia 7,14 hadi 79. 4,982.77, ikikwepa mwelekeo wa kuendelea kushuka.

Soko la Nasdaq Composite ambalo ni muhimu sana kwa kampuni za kiteknolojia liliporomosha pointi 335.35, au asilimia 2.15, hadi 15,267.91.

Sekta zote kuu 11 za S&P 500 (kampuni bora 500 zinazouza hisa kwenye soko la Marekani) ziliishia kwenye rangi nyekundu. Kampuni za nyenzo na vitu vya manunuzi ya matumizi zimeongoza hasara, zikiwa chini kwa asilimia 2.96 na asilimia 2.54, mtawalia. Kampuni za mambo ya fedha zimeshuhudia kushuka kidogo, zikitulia asilimia 0.41.

Masoko yaliruka juu wakati wa kipindi cha ufunguzi wa mauzo ya hisa, huku baadhi ya wafanyabiashara wakirejelea hali ya mauzo ya kupita kiasi na matumaini juu ya uwezekano wa kufanya mazungumzo na wenzi wakuu wa kibiashara juu ya ushuru.

Hisia za soko zilipata msukumo wa muda mfupi baada ya Rais wa Marekani Trump kuchapisha kwenye Mtandao wa True Social kuhusu "mazungumzo mazuri ya simu" na Kaimu Rais wa Korea Kusini, na Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent kukiambia kituo cha utangazaji cha CNBC kwamba nchi takriban 70 zimeshawasiliana na Marekani kutafuta mazungumzo ya ushuru.

Wafanyabiashara wakifanya kazi kwenye sehemu ya miamala ya Soko la Hisa la New York mjini New York, Marekani, Aprili 8, 2025. (Picha na Michael Nagle/Xinhua)

Wafanyabiashara wakifanya kazi kwenye sehemu ya miamala ya Soko la Hisa la New York mjini New York, Marekani, Aprili 8, 2025. (Picha na Michael Nagle/Xinhua)

Hata hivyo, mauzo hayo mazuri yalififia haraka baada ya Ikulu ya White House kuthibitisha kwamba itakuwa ikisonga mbele na mapendekezo ya kuongeza asilimia 50 ya ushuru kwa bidhaa za China, hatua ambayo ilizidisha kwa kiasi kikubwa mtanzuko wa kibiashara na kuyumbisha imani ya wawekezaji.

Hatua hiyo itapandisha kiwango cha jumla cha ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China hadi asilimia 104, ikizua wasiwasi wa wawekezaji juu ya mvutano wa kibiashara na kuzorota kwa uchumi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha