China yachukua hatua haraka kutuliza masoko huku kukiwa na msukosuko wa kifedha duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2025

BEIJING - China imeanzisha mfululizo wa hatua za haraka na madhubuti za kutuliza soko la mitaji na kurejesha imani ya wawekezaji kutokana na kutokea kwa msukosuko wa kifedha wa kimataifa uliosababishwa na ushuru uliotozwa na Marekani dhidi ya wenzi wake wa kibiashara.

Soko la hisa la China lilifungwa katika kiwango cha juu zaidi jana Jumanne, likiongezeka kutoka kwenye hasara kubwa katika siku ya awali ya biashara, kufuatia hatua mbalimbali zilizotangazwa na mamlaka za kifedha, pamoja na hatua ratibiwa za kampuni za uwekezaji zinazomilikiwa na serikali, kampuni za serikali (SOEs) na kampuni za bima.

Jana Jumanne, kiwango cha jumla cha kigezo cha soko la hisa la Shanghai kilipanda kwa asilimia 1.58 na kiwango hicho cha soko la hisa la Shenzhen kilipanda kwa asilimia 0.64. Kiwango cha Soko la hisa la ChiNext, kilipanda kwa asilimia 1.83.

Kampuni za uendeshaji mitaji zinazomilikiwa na serikali ya China zimechukua hatua haraka kuongeza umiliki wao wa hisa za ndani, zikitoa imani kubwa katika mtazamo wa muda mrefu wa soko la mitaji nchini humo. Benki Kuu ya China, pia imetangaza uungaji mkono wa kiukwasi kupitia uwezeshaji wa kukopesha tena siku hiyo ya Jumanne.

Kampuni ya Uwekezaji ya Central Huijin, kampuni ya uwekezaji inayomilikiwa na serikali ya China, imesema kwa mara nyingine tena imeongeza umiliki wake wa mfuko unaolingana na kiwango cha soko la hisa na itaendelea kufanya hivyo katika siku zijazo ili "kulinda kithabiti" uendeshaji imara wa soko la mitaji.

Kufuatia taarifa hiyo ya Central Huijin, benki kuu ya China imeahidi kuunga mkono kampuni hiyo kwa uthabiti katika kuongeza umiliki wake wa mfuko unaolingana na kiwango cha soko la hisa na itatoa uungaji mkono wa kutosha wa kukopesha tena inapobidi.

Kamisheni ya Usimamizi na Udhibiti wa Mali inayomilikiwa na Serikali ya Baraza la Serikali la China imesema siku hiyo ya Jumanne kwamba inaunga mkono kikamilifu mashirika ya serikali kuu katika kupanua kununua hisa zao sokoni ili kulinda haki za wanahisa na kuimarisha imani ya soko.

Mashirika kadhaa ya serikali ya China yameanzisha mipango ya kununua wa hisa zao sokoni, yakisisitiza imani yao thabiti katika matarajio ya muda mrefu ya uchumi na soko la mitaji la nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha