

Lugha Nyingine
China kushirikiana na EU kuhimiza maendeleo mazuri na thabiti ya uhusiano kati yao
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema katika mazungumzo ya simu na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen siku ya Jumanne kwamba China inapenda kufanya kazi na Ulaya ili kuhimiza maendeleo mazuri na thabiti ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya na kwamba uhusiano kati ya China na EU unaonyesha mwelekeo wa kuendeleza kwa madhubuti.
"Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Umoja wa Ulaya, na maendeleo ya uhusiano wa pande mbili yanakabiliwa na fursa muhimu," amesema, akibainisha kuwa Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo ya simu na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa mwanzoni mwa mwaka huu, ambayo yanatoa dira ya kuzidisha uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
China na EU ni wenzi muhimu zaidi wa kibiashara wa kila upande, amesema, akiongeza kuwa uchumi wao unawiana sana na maslahi yanaingiliana kwa karibu.
Li ameahidi nia ya China ya kushirikiana na Umoja wa Ulaya kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano wa kivitendo, na kutatua masuala yanayofuatiliwa ya kila mmoja wao kwa njia ya mazungumzo na mashauriano.
“Pande hizo mbili zinapaswa kuhimiza kufanyika kwa mazungumzo mapya ya ngazi ya juu kati ya China na Umoja wa Ulaya katika nyanja za kimkakati, kiuchumi na kibiashara, kijani na kidijitali mapema iwezekanavyo,” amesema.
Li amebainisha kuwa hivi karibuni Marekani imetangaza kutoza ushuru kwa wenzi wake wote wa kibiashara, ikiwa ni pamoja na China na Umoja wa Ulaya, kwa visingizio mbalimbali, jambo ambalo kimsingi ni maamuzi ya upande mmoja, kujihami kibiashara na ukandamizaji kiuchumi.
“Hatua madhubuti zinazochukuliwa na China si tu kwa ajili ya kulinda mamlaka, usalama na maslahi yake ya maendeleo bali pia kutetea utaratibu wa biashara ya kimataifa na haki na usawa wa kimataifa,” Li amesema, akiongeza kuwa binadamu wote wanaishi katika kijiji kimoja cha dunia na hakuna nchi inayoweza kustawi kwa kujitenga.
Kujihami kibiashara hakuelekei popote, na uwazi na ushirikiano pekee ndiyo unaowakilisha njia sahihi kwa binadamu,” Li ameongeza.
Akisema kuwa EU daima inaweka umuhimu mkubwa kwa uhusiano wake na China, von der Leyen amesema ni muhimu kwa sasa kudumisha endelevu na utulivu wa uhusiano wa EU na China.
"Upande wa Ulaya unatarajia kufanya mkutano mpya wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na China kwa wakati mwafaka ili kupitia upya yaliyopita, kuangalia siku zijazo, na kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya EU na China," alisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma