China yahuisha sera ya kurejesha malipo ya kodi kwa watalii wa kigeni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2025
China yahuisha sera ya kurejesha malipo ya kodi kwa watalii wa kigeni
Picha hii ya faili isiyo na tarehe ikionyesha mtalii wa kigeni akipiga picha na mhudumu aliyevalia mavazi ya kijadi kwenye duka la kwanza kabisa la Quanjude katika Mtaa wa Qianmen mjini Beijing. (Xinhua)

BEIJING - China imehuisha sera yake ya kurejesha malipo ya kodi kwa watalii wa kigeni kutoka kurejesha malipo hayo ya kodi wakati wa kuondoka kuwa ya kurejesha malipo hayo mara tu baada ya kununua bidhaa, Mamlaka ya Ushuru ya Serikali ya China (STA) imetangaza jana Jumanne.

Chini ya sera hiyo mpya ya kurejesha malipo ya kodi baada ya kununua, watalii wa kigeni wanaweza kudai papo hapo punguzo la kodi ya thamani ya nyongeza (VAT) katika maduka yasiyolipishwa kodi, na kuwawezesha kutumia tena kiasi kilichorejeshwa katika wakati wa kufanya manunuzi zaidi.

Hapo awali, mapunguzo ya VAT yalipatikana tu kwa kutolewa kutoka kwenye akaunti wakati watalii wa kigeni wakiondoka nchini China.

“Mabadiliko hayo ya sera, yaliyojaribiwa hapo awali mjini Shanghai, Beijing, Guangdong, Sichuan na Zhejiang, sasa yamekidhi mahitaji yote ya uendeshaji kwenye maeneo yote nchini China,” mamlaka hiyo imesema.

Ofisa kutoka STA amesisitiza dhamira yao ya kuimarisha mwongozo wa sera na kurahisisha taratibu za kurejesha malipo hayo ya kodi.

Li Xuhong, naibu mkuu na profesa katika Chuo kikuu cha Uhasibu cha Kitaifa cha Beijing, amesema kuwa utekelezaji wa mpango huo wa huduma nchini kote utainua kiwango cha huduma ya utalii ya China na kujenga mazingira ya utalii yaliyo "rafiki, ufanisi na rahisi".

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha