

Lugha Nyingine
Mchumi wa Zambia aonya kuwa kupanda kwa ushuru wa Marekani kunavuruga utulivu wa dunia
Mchumi wa kijamii wa Zambia Kelvin Chisanga, ameonya kuwa ongezeko kubwa la ushuru wa Marekani kwa washirika wake wakuu wa kibiashara linatarajiwa kusababisha athari hasi za kimataifa na kusambaa kwa ukosefu wa utulivu.
Chisanga amesema hatua hiyo inaashiria kuwa uhasama wa kibiashara unaongezeka zaidi, na matokeo yake yanazidi matarajio ya awali.
Ametahadharisha kuwa kupanda huko kwa ushuru tayari kumeleta mshtuko katika masoko ya kimataifa na kuondoa imani ya wawekezaji.
Ameongeza kwa kusema kuwa tozo za ushuru huo zinapunguza mahitaji ya bidhaa muhimu kama vile mafuta na shaba, na kwamba hii ilikuwa ndio sababu kuu ya mauzo ya dhamana za Afrika yaliyoshuhudiwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Ameonya zaidi kwamba sera sawia zinazopitishwa na maeneo yaliyoathirika zinaweza kufanya mambo kuwa mabaya zaidi na kusababisha vita vya kibiashara duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma