

Lugha Nyingine
Algeria yafunga anga yake kwa Mali baada ya tukio la droni
Algeria jana Jumatatu ilitangaza kufunga anga yake kwa ndege zote za Mali, kufuatia ukiukwaji wa mara kwa mara wa mamlaka yake ya ardhi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Algeria, uamuzi huo utatekelezwa kwa ndege zote zinazokwenda na kutoka Mali. Hatua hiyo inamaanisha kupamba moto kwa mvutano kati ya Algeria na Mali, ulioanza Jumapili baada ya Mali na washirika wake Niger na Burkina Faso kuwarudisha mabalozi wao nchini Algeria ili kupinga tukio la kuangushwa kwa droni ya kijeshi ya Mali na jeshi la Algeria kati ya Machi 31 hadi Aprili 1.
Serikali za nchi hizo tatu, kupitia taarifa ya pamoja, zimelaani vikali tukio hilo la droni, zikilitaja kama “kitendo cha uhasama kilichopangwa” na Algeria na kwamba “kilivuruga operesheni dhidi ya kundi moja linalopanga shambulizi la kigaidi”.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria pia imejibu kwa kutoa taarifa mapema siku hiyo ikilaani shutuma hizo ambazo imezitaja kama “kali, za kimakosa na zisizo na msingi” na kusema kwamba droni ya Mali iliangushwa kwa kuwa ilivamia anga ya Algeria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma