

Lugha Nyingine
Madaktari wa China waandaa zahanati zinazohamishika kaskazini mwa Tanzania
Timu za madaktari wa China nchini Tanzania Jumapili ziliandaa shughuli za siku mbili za kutoa matibabu bure kupitia zahanati zinazohamishika mjini Arusha nchini Tanzania, ikiwa ni hatua yao ya kuadhimisha Siku ya Afya Duniani, inayoangukia Aprili 7.
Zahanati hiyo iliandaliwa na kushirikiwa na timu ya 27 ya madaktari wa China waliopo Tanzania bara, timu ya 34 ya madaktari wa China visiwani Zanzibari, na timu ya udhibiti wa kichocho kutoka mradi wa Ushirikiano wa China katika kisiwa cha Pemba.
Wataalamu 13 wa matibabu wa China walitoa huduma bila malipo, ikiwemo mihadhara ya afya, upimaji wa afya, na michango ya dawa.
Zahanati hiyo ilitoa huduma kwa wafanyakazi zaidi ya 200 wa Tanzania na China wa Kundi la Uhandisi na Ujenzi wa Reli la China wanaofanya kazi katika mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu huko Arusha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma