

Lugha Nyingine
Tanzania na DRC zakubaliana kuendeleza bandari kavu ili kuimarisha biashara ya kikanda
Picha hii iliyopigwa Septemba 22, 2023, ikionyesha bandari ya Dar es Salaam iliyoko Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Dong Jianghui)
DAR ES SALAAM - Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimetia saini makubaliano ya kuendeleza bandari kavu katika nchi hizo mbili, hatua hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara wa kikanda.
Makubaliano hayo yaliyotiwa saini Jumamosi mjini Lubumbashi, DRC, yanaeleza kuwa kila nchi itatoa ardhi kwa ajili ya kujenga miundombinu ya bandari kavu ili kuongeza ufanisi wa kupakia na kupakua mizigo na kusafirisha bidhaa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi nchini Tanzania Godius Kahyarara amesema mpango huo unafuatia kuongezeka kwa asilimia 180 kwa mizigo inayopelekwa DRC kupitia bandari ya Dar es Salaam katika miaka minne iliyopita.
Ameyapongeza makubaliano hayo kuwa ni hatua muhimu katika utekelezaji wa makubaliano ya pande mbili wa maendeleo ya miundombinu wa mwaka 2022.
Picha hii iliyopigwa Mei 11, 2023 ikionyesha mwonekano wa Kinshasha, Mji Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokraia ya Kongo. (Xinhua/Han Xu)
Chini ya makubaliano hayo, Tanzania itapokea ardhi kwa ajili ya kujenga bandari kavu za Kasumbalesa, Kasenga, na Kalemie nchini DRC. Katika kuilipa, DRC itatenga ardhi kwa ajili ya maendeleo ya bandari kavu katika maeneo ya Kwala na Katosho nchini Tanzania.
Kahyarara amesema kuwa mradi wa bandari kavu utakaotekelezwa chini ya mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma