Trump na Netanyahu wajadili mateka wa Gaza na ushuru kwenye Ikulu ya White House

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2025

Rais Donald Trump wa Marekani (katikati) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia) katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 7, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Rais Donald Trump wa Marekani (katikati) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia) katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 7, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

WASHINGTON - Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekutana katika Ikulu ya White House jana ya Jumatatu, wakijikita katika mzozo wa mateka wa Gaza na ushuru unaotozwa na Marekani kwa bidhaa za Israel ambapo kwenye mkutano mfupi katika Ofisi ya Oval uliokuwa wazi kwa waandishi wa habari, Trump ametaja kuachiliwa huru mateka wanaoshikiliwa Gaza kuwa "kipaumbele cha juu." Akionyesha matumaini kuhusu majadiliano yanayoendelea lakini hakutoa maelezo zaidi.

"Tunapiga hatua," Trump amesema. "Naamini tutawaona mateka wote nyumbani hivi karibuni."

Netanyahu alikubaliana naye, akisisitiza dhamira ya Israeli kuwaachilia huru mateka hao.

Pia wamezungumzia kuhusu usimamishaji mapigano usio imara kati ya Israel na Hamas. Ingawa wametangaza hakuna makubaliano mapya, wote wamesisitiza umuhimu wa kupunguza ghasia katika eneo hilo.

Trump ametetea sera yake ya ushuru iliyotolewa hivi karibuni wa asilimia 17 kwa bidhaa kutoka Israel, sehemu ya sera yake pana ya biashara inayoathiri makundi mengi ya uchumi.

Netanyahu iliripotiwa kuwa alikuwa akitafuta msamaha kutokana na ushuru huo, akisisitiza juhudi za Israel za kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Marekani.

Mwaka 2024, jumla ya thamani ya biashara ya bidhaa kati ya nchi hizo mbili ilikadiriwa kuwa dola za Kimarekani bilioni 37.0, huku mauzo ya nje ya Marekani kwa Israeli yakiwa dola bilioni 14.8 na uagizaji bidhaa kutoka Israeli ukiwa dola bilioni 22.2, ikisababisha nakisi ya biashara ya Dola za Kimarekani bilioni 7.4.

Ziara hiyo ya Netanyahu katika Ikulu ya White House ilipangwa kwa njia ya simu Alhamisi wiki iliyopita kati ya viongozi hao wawili wakati Netanyahu alipoibua suala hilo la ushuru, kwa mujibu wa maafisa wa Israel.

Ikulu ya White House hapo awali ilikuwa imepanga mkutano wa pamoja na waandishi wa habari lakini ikaufuta bila maelezo. Badala yake, waandishi wa habari waliuliza maswali wakati walipohudhuria kwa muda mfupi wa mkutano huo kwenye Ofisi ya Oval.

Trump hakujadili mipango yoyote ya muda mrefu ya kuijenga upya Gaza kwenye mkutano huo. Utawala wake hapo awali ulipendekeza mawazo tata kwa eneo hilo, ambayo yamekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa makundi mbalimbali.

Mkutano huo umeangazia uhusiano wenye changamoto kati ya Marekani na Israel, kuwianisha masuala ya usalama na maslahi ya kiuchumi. Viongozi wote wawili wameahidi kuendelea kushirikianai kwa karibu katika masuala hayo.

Rais wa Marekani Donald Trump (katikati) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia) katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 7, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Rais wa Marekani Donald Trump (katikati) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia) katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 7, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha