

Lugha Nyingine
Vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga nchini China vyaendelea kupungua
Muuguzi akifanya kazi kwenye hospitali ya huduma ya afya ya mama na mtoto katika Mji wa Huai'an, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Mei 12, 2024. (Picha na Zhao Qirui/Xinhua)
BEIJING – Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kamati ya kitaifa ya afya ya China, katika Mwaka 2024, kiwango cha vifo vya mama wajawazito kilifikia 14.3 kwa kila mama wajawazito 100,000 waliojifungua, na kiwango cha vifo vya watoto wachanga kilifikia 4 kwa kila watoto 1,000 waliozaliwa, na kiwango cha vifo vya watoto kifikia 5.6 kwa kila watoto 1,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Katika miaka ya hivi karibuni, hali ya afya ya mama na mtoto nchini China imeendelea kuboreshwa, ambapo vifo vya mama wajawazito wanaojifungua vimepungua kwa wastani wa asilimia 4 hivi kila mwaka, na vifo vya watoto wachanga na vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kwa wastani wa asilimia 5 hivi kila mwaka. Na pia mafanikio makubwa yamepatikana katika kuzuia na kutibu magonjwa makubwa yanayoathiri wanawake na watoto. Imesema, katika miaka mitano iliyopita, vifo vya watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na kasoro za kuzaliwa vimepungua kwa zaidi ya asilimia 30.
Aidha, matukio ya kasoro kali na za kulemaa wakati wa kuzaliwa, kama vile kasoro za neural tube na Down syndrome, yamepungua kwa asilimia 21 huku hali ya maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto pia imepungua, kwa sasa imefikia asilimia 1.3.
"Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na maboresho yanayoendelea katika mfumo wa huduma ya afya ya mama na mtoto nchini China".
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kamati ya Kitaifa ya Afya, China sasa imekuwa na vituo 3,491 vya matibabu kwa wajawazito walio katika hali mbaya, vituo 3,221 vya watoto wachanga wenye hali mahututi, na vituo 3,081 vya afya ya mama na mtoto. Imesema, idadi ya madaktari wa uzazi na watoto nchini kote China imefikia 373,000.
Hadi kufikia mwisho wa mwaka 2023, idadi ya madaktari wa watoto iliongezeka hadi 234,000, idadi ya vitanda vya hospitali kwa kila watoto 1,000 imeongezeka hadi 2.55, ikiwa ni ongezeko la 0.62 ikilinganishwa na mwaka 2015. Aidha, zaidi ya asilimia 90 ya taasisi za afya za msingi sasa zimekuwa na vifaa vya kutoa huduma za watoto.
China pia imeeneza utaalamu wake nje ya nchi ambapo timu za madaktari wa China zilizotumwa zimetoa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika nchi na maeneo 44, zikiwemo Morocco na Ethiopia huku mwaka 2024 pekee, timu hizo zikisaidia kuzaliwa watoto 63,800.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma