

Lugha Nyingine
China yasema Marekani kuweka "ushuru wa Reciprocal" kunanyima nchi, hasa za Kusini, haki ya maendeleo
BEIJING – Marekani kuweka kwa upande mmoja "ushuru wa Reciprocal" kunazinyima kikamilifu nchi, haswa zile za Kusini, haki yao ya maendeleo, na hakika itakabiliwa na upingaji mkubwa kutoka jumuiya ya kimataifa, Lin Jian, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema.
Hivi karibuni, Marekani imeweka ushuru kwa wenzi wake wote wa kibiashara, ukiathiri nchi na kanda zaidi ya 180 duniani kote, ikiwa ni pamoja na baadhi ya nchi zilizoainishwa kama nchi zilizoko nyuma maendeleo zaidi na Umoja wa Mataifa. Wachambuzi wameeleza kwamba ushuru huo wa juu utaleta athari isiyokuwa ya kawaida na kali kwa nchi maskini yenye miundo rahisi ya kiuchumi na utegemezi mkubwa kwa mauzo ya nje.
Akijibu swali husika, msemaji Lin amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatatu kwamba Marekani, chini ya kivuli cha "kutendeana kwa usawa," imetenda kwa namna ambayo inatanguliza maslahi yake kwa gharama ya faida halali ya nchi nyingine. Amesema, kitendo hicho kinaiweka "Marekani Kwanza" juu ya sheria za kimataifa, ikitoa mfano wa hatua za upande mmoja, kujihami kiuchumi, na uonevu wa kiuchumi.
Lin ameongeza kuwa serikali ya China imetoa msimamo wake juu ya kupinga matumizi hayo mabaya ya ushuru ya Marekani.
Amesema, uchambuzi wa takwimu kutoka Shirika la Biashara Duniani unaonyesha kuwa, chini ya kuwepo tofauti za uchumi na kutokuwa na usawa wa nguvu, sera hizo za ushuru za Marekani zitazidisha pengo la utajiri kati ya nchi, huku nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zikikabiliwa na athari mbaya zaidi. Ameeleza kuwa, mmwelekeo huo unaleta tishio kubwa kwa juhudi kusudiwa kufikia Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 kwa ajili ya Maendeleo Endelevu.
“Hatua ya Marekani ya kuweka viwango tofauti vya ushuru inakiuka kanuni ya Shirika la Biashara Duniani ya kutobagua, kudhoofisha kwa kiasi kikubwa utaratibu wa kawaida wa kimataifa wa uchumi na biashara, vilevile usalama na utulivu wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na usambazaji,” Lin amesema, akiongeza kuwa hatua hiyo inaharibu kwa kiasi kikubwa mfumo wa biashara wa pande nyingi, inaleta tishio kubwa kwa mchakato wa kuimarisha uchumi wa dunia, na inatarajiwa kukutana na upingaji mkubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.
Amesema, kufungua mlango na ushirikiano ni mwelekeo wa kihistoria, na kunufaishana ni matarajio ya watu na kwamba maendeleo ni haki ya wote kwa nchi zote, si upendeleo wa wachache.
Amesisitiza kuwa, nchi zote zinapaswa kushikilia kanuni ya mazungumzo ya kina, mchango wa pamoja na kunufaika pamoja, kutilia maanani uhusiano wa kweli wa pande nyingi, kwa pamoja kupinga aina zote za uamuzi wa upande mmoja na kujihami, na kushikilia mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa ukiwa ndiyo msingi wake na mfumo wa biashara wa pande nyingi huku Shirika la Biashara Duniani likiwa msingi wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma