Je, huu ni "ushuru wa kulipiza kisasi" au "matumizi mabaya ya ushuru wa jumla"?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 07, 2025

Machi 2, kwa saa za Marekani Mashariki, Marekani ilitangaza kuweka "ushuru wa Reciprocal" kwa wenzi wake wote wa kibiashara. Sera hiyo, kwa jina la kile kinachoitwa "kutendeana kwa usawa", inachukua mbinu ya "ushuru wa kiwango cha kimataifa" na "nchi moja, kiwango kimoja cha ushuru ", ikijaribu kushughulikia kile kinachoitwa "biashara isiyo ya haki" ya nchi nyingine kwa kurekebisha viwango vya ushuru kwa upande mmoja.

Kwa ufafanuzi, "ushuru wa Reciprocal" si ushuru halisi, wala hauko kwa usawa. Kile kinachoitwa "ushuru wa Reciprocal" unapatikana kwa mahesabu kulingana tu na kiwango cha nakisi ya biashara ya Marekani na wenzi wake wakuu wa kibiashara katika biashara ya Marekani kuagiza bidhaa kutoka nchi hizo.

Si viwango halisi vya ushuru, bali mkandamizaji wa hatua za upande mmoja. Chini ya uelewa rahisi na mbaya wa upande wa Marekani, Marekani itaweka ushuru sawa kwa upande mwingine kadri upande huo husika utakavyoweka ushuru kwa Marekani. Ukweli ni kwamba, "kutendeana kwa usawa" inamaanisha si tu usawa, lakini pia kunufaishana.

Kwa mtazamo wa sheria, "ushuru wa Reciprocal" unakiuka sheria za kimataifa. WTO inatoa hadhi maalum na tofauti kwa nchi zinazoendelea, ikiziwezesha kuongeza ushuru wa forodha. Wakati huo huo, kwa mujibu wa Makubaliano ya Jumla ya Ushuru na Biashara chini ya mfumo wa WTO, ahadi za kupunguza ushuru zinazoamuliwa na nchi wanachama kupitia mazungumzo ya pande nyingi ni zenye nguvu za kisheria, na hakuna nchi mwanachama inaweza kuongeza ushuru kiholela bila makubaliano.

Uamuzi huo wa Marekani wa upande mmoja kuhusu viwango vya ushuru kwa bidhaa kutoka nchi nyingine unakiuka kanuni hiyo ya hadhi ya nchi zinazopendelewa zaidi na wajibu wa kufungwa kiushuru, na ni kutozingatia kanuni za pande nyingi.

Kutoka kwenye mtazamo wa matokeo, "ushuru wa Reciprocal" hauna faida bali hasara. "Ushuru wa Reciprocal" huanzisha vita vya kibiashara vya kimataifa na kuvunja mfumo wa usambazaji bidhaa wa "kunufaishana", ambayo itasababisha kupungua kwa uchumi na biashara ya dunia na kusababisha mdororo wa kiuchumi. Si tu kwamba itaathiri vibaya nchi nyingi zinazoendelea, lakini pia itarudisha nyuma uchumi wa Marekani.

Ripoti ya Mtazamo wa Uchumi Duniani iliyotolewa na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) inaamini kuwa kutokana na kutokuwa na uhakika kwa sera ya ushuru ya Marekani, ukuaji wa uchumi duniani utapungua zaidi, na makadirio ya kiwango cha ukuaji wa uchumi duniani kwa mwaka 2025 na 2026 yatapunguzwa kwa asilimia 0.2 na 0.3 hadi 3.1% na 3.0%, mtawalia.

Ajabu, neno la Kiingereza “reciprocal”, pamoja na maana ya kawaida ya "kunufaishana, kutendeana kwa usawa", pia linamaanisha "kurudi nyuma (reverse), kutendana kinyume (mutual inverse)". Kile kinachoitwa "ushuru wa Reciprocal" wa Marekani kwa kweli ni matumizi mabaya ya umwamba na kutumia fimbo ya ushuru. Wataalam wengine wanaitafsiri kama "matumizi mabaya ya ushuru wa jumla".

Mwaka 1930, Marekani ilianzisha Sheria ya Ushuru ya Smoot-Hawley, ambayo ilijaribu kulinda viwanda vya ndani kwa kuweka ushuru, lakini vita vya ushuru ilivyovisababisha hatimaye vilizidisha hali mbaya ya kudidimia kwa uchumi wake.

Sauti bado iko masikioni mwetu, na hatupaswi kusahau yaliyopita. Inabidi kuachana na haya "matumizi mabaya ya ushuru wa jumla" ambayo ni dhidi ya utandawazi wa uchumi duniani na kinyume na upendeleo wa watu duniani, na ipasavyo kutatua tofauti na wenzi wake wa biashara kwa njia ya mazungumzo ya usawa. Hii ndiyo njia sahihi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha