

Lugha Nyingine
China kuimarisha udhibiti wa mauzo ya nje ya vitu vya madini adimu kunaonyesha dhamira ya kulinda usalama wa taifa
BEIJING - Hatua za China za kudhibiti mauzo ya nje ya baadhi ya vitu vinavyohusiana na madini adimu zimeonyesha dhamira yake thabiti ya kudumisha amani na usalama wa dunia, Shirikisho la Viwanda vya Metali zisizo za Chuma la China imesema jana Jumapili.
Hayo yamekuja baada ya Wizara ya Biashara ya China na Mamlaka Kuu ya Forodha ya China siku ya Ijumaa kutangaza hatua za kudhibiti mauzo ya nje ya vitu vinavyohusiana na aina saba za madini adimu ya uzito wa kati na mkubwa.
Vitu hivyo vinavyohusiana na madini adimu vina matumizi ya kijeshi na ya kiraia, shirikisho hilo limesema, likiongeza kuwa hatua hizo zimezingatia kikamilifu hatua zinazotekelezwa za kimataifa.
“Maadamu kampuni hazijihusishi na shughuli zinazodhoofisha mamlaka ya taifa, usalama, au maslahi ya maendeleo ya China, hatua hizo hazitaathiri uendeshaji wao wa kawaida na shughuli za biashara, achilia mbali utulivu na usalama wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na usambazaji,” shirikisho hilo limesema.
Pia limeongeza kuwa kampuni za madini adimu za China, kwa kulingana na matakwa ya tangazo hilo la Ijumaa, zitasisitiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu zaidi na kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na nchi marafiki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma