

Lugha Nyingine
China yatoa mwongozo mpya wa kuimarisha utaratibu wa usimamizi wa bei
BEIJING - China kupitia Ofisi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Ofisi ya Baraza la Serikali la China imetoa mwongozo wa kuzidisha mageuzi ya bei na kuboresha utaratibu wa usimamizi wa bei.
Unalenga kuboresha utaratibu wa upangaji bei sokoni ili kuhimiza upangaji rasilimali kwa ufanisi, utaratibu wa mwongozo wa bei kwenye maeneo muhimu ya maendeleo na usalama, utaratibu wa kusimamia bei ili kuwa na viwango mwafaka vya bei, na utaratibu wenye uwazi na kutabirika wa usimamizi wa bei za soko.
“China itaimarisha utaratibu wa upangaji bei sokoni kwa kuimarisha mageuzi ya bei inayolingana na soko, kuharakisha ujenzi wa soko wa maeneo muhimu na kuweka mazingira ya soko yenye ushindani na yenye utaratibu” mwongozo huo unasema.
Mwongozo huo utalenga maeneo matano muhimu: bidhaa za kilimo ili kuhakikisha usalama wa chakula, bei ya nishati kuunga mkono mageuzi ya nishati kuwa ya kijani, huduma za umma zinazosaidia maendeleo endelevu, huduma za umma kwa ufikiaji wa usawa, na mbinu za kupanga bei kwa matumizi salama na bora ya data ya umma.
Udhibiti juu ya kiwango cha jumla cha bei utaimarishwa kupitia uwiano bora kati ya sera za bei na sera za bajeti, za fedha, za viwanda na za ajira, mwongozo huo unaeleza, ukiongeza kuwa, juhudi zitafanywa ili kuimarisha utulivu wa bei za bidhaa muhimu.
Mwongozo huo, utaboresha zaidi utaratibu wa usimamizi wa bei sokoni, kuweka mazingira ya wazi na yenye kutabirika ya usimamizi kwa mashirika ya biashara, na kulinda haki na maslahi halali ya watumiaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma