

Lugha Nyingine
Fujian, China: Mwamba na Macheo katika Kijiji cha Aojiao
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 02, 2025
Kijiji cha Aojiao ni kijiji cha wavuvi kinachopatikana katika Wilaya ya Dongshan, Mji wa Zhangzhou wa Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. Kinazungukwa na bahari katika pande tatu, na kina mandhari nzuri sana. Kama ukipanda kilima nyuma ya ufukwe na kusimama kwenye mwamba ambapo kuna mnara wa taa, utakuwa na uwezo wa kutazama uso mzima wa bahari na kusubiri macheo. Meli za uvuvi ambazo zilikuwa zimetia nanga kwenye gati la kijiji hicho zipo tayari kutoka, na uso wa bahari tulivu hatua kwa hatua unakuwa wa hali motomoto kadri macheo yanapotokea.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma