

Lugha Nyingine
China na Afrika Kusini zaongoza kwa uwekezaji wa kigeni nchini Namibia
(CRI Online) April 02, 2025
Ripoti ya mwaka iliyotolewa na Benki ya Namibia imesema, China na Afrika Kusini zimeongoza kwa vyanzo vya uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini Namibia kwa mwaka 2024.
Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatatu wiki hii imesema, sekta za madini na fedha zimepokea uwekezaji mkubwa zaidi, huku sekta ya madini ikichukua asilimia 67.7 ya mchango wa jumla wa uwekezaji huo.
Hata hivyo, Benki hiyo imesema, hisa za China na Afrika Kusini katika uwekezaji zilishuka kidogo kutokana na wawekezaji wapya, haza nchi za Ghuba ya Uarabuni, Marekani na Ufaransa ambazo zimeongeza uwepo wao katika shughuli za utafiti wa mafuta na gesi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma