

Lugha Nyingine
Rais Putin ahimiza Russia na China kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati
MOSCOW - Rais Vladimir Putinwa Russia siku ya Jumanne alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Russia katika Ikulu ya Kremlin ametoa wito kwa Russia na China kuimarisha zaidi ushirikiano wao wa kimkakati chini ya hali ya msukosuko duniani.
Katika mkutano huo, Rais Putin amewasilisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi Jinping wa China na kueleza kuridhishwa na utekelezaji mzuri wa maafikiano yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili.
Amebainisha kuwa uhusiano kati ya Russia na China unaendelea kuimarika katika ngazi ya juu, huku ushirikiano wa kivitendo ukizidishwa katika sekta mbalimbali na "Mwaka wa Utamaduni wa Russia na China" unaoendelea ukitoa kihamasa uungaji mkono wa umma, ikiimarisha zaidi msingi wa urafiki kati ya pande mbili.
Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu ushindi wa Umoja wa Kisovieti katika Vita Vikuu vya Kizalendo, Putin ametoa mwaliko kwa wajumbe wa China kushiriki shughuli mbalimbali nchini Russia.
Amesisitiza umuhimu wa pamoja wa kihistoria kusherehekea ushindi dhidi ya ufashisti wa Nazi na ubabe wa kijeshi wa Japan, akisema kwamba Russia inafanya maandalizi kamili kwa shughuli hiyo.
Ameongeza kuwa hatua hii inapaswa kusukuma ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya Russia na China kufikia ngazi mpya na kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi ndani ya mifumo kama vile Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na BRICS.
Kuhusu msukosuko duniani, Putin amesisitiza haja ya nchi zote mbili kutuma ishara imara ya kuimarishwa kwa uratibu wa kimkakati kwa dunia.
Kwa upande wake Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amewasilisha salamu kutoka kwa Rais Xi Jinping wa China kwa Rais Putin.
Amesisitiza kuwa chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu hao wawili, uhusiano kati ya China na Russia umekomaa kuwa ushirikiano himilivu na thabiti wenye sifa ya kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa, uwiano wa karibu wa kimkakati, na ushirikiano endelevu wa kivitendo.
Amebainisha kuwa, ushirikiano huu, umelinda maendeleo ya nchi zote mbili na maslahi ya pamoja katika masuala makubwa ya kimataifa na kikanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma