

Lugha Nyingine
Tamasha la 42 la Utamaduni wa Maua ya Peony la Luoyang, China laanza rasmi
Tamasha la 42 la Utamaduni wa Maua ya Peony la Luoyang limefunguliwa rasmi jana Jumanne, Aprili 1 katika Mji wa Luoyang, Mkoa wa Henan, katikati mwa China. Tamasha hilo la mwaka huu litafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 15, Aprili, na muda wa kutazama maua utadumu kwa mwezi mmoja.
Tamasha hilo zima linahusu "maua ya peony" kama mhusika mkuu, likiunganisha vizuri mambo kama vile mavazi ya Hanfu, muziki, shughuli za nje, na matumizi ya manunuzi. Limeandaa shughuli 10 kuu na matukio unganishi 35, likilenga kuwasilisha tamasha la kitamaduni la kipekee na lenye uhondo kwa watalii.
Mji huo wa Luoyang pia umejenga maeneo tisa ya kipekee ya matumizi ya usiku kwenye eneo la kati la mjini, ukianzisha shughuli za usiku kama vile: utalii wa kuona mandhari na mapumziko, burudani za kitamaduni, vyakula vya kipekee, na manunuzi ya mitindo...ikifanya usiku wa Luoyang kuwa wa shamrashamra, na kusukuma ujumuishi wa mambo mbalimbali ya muundo wa matumizi ya usiku.
Bustani ya Mimea ya Masalio ya Mji Mkuu wa Enzi za Sui na Tang mjini Luoyang, Mkoa wa Henan, China. (Picha na Idara ya Uenezi ya Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Manispaa ya Luoyang)
Muonekano ya maoyesho. (Picha na Idara ya Uenezi ya Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Manispaa ya Luoyang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma