Xi Jinping aongoza mkutano wa viongozi kuhusu vifungu vya ukaguzi wa ulinzi wa mazingira na ukaguzi wa nidhamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2025

BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China na katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ameongoza mkutano wa viongozi wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ili kupitia seti moja ya vifungu vya ukaguzi wa ulinzi wa mazingira ya ikolojia.

Mkutano huo uliofanyika jana Jumatatu, pia umepitia ripoti ya raundi ya nne ya ukaguzi wa nidhamu iliyoanzishwa na Kamati Kuu ya 20 ya CPC.

Mkutano huo umesema ukaguzi wa kazi ya ulinzi wa mazingira ya ikolojia umepata matokeo ya kuhimiza juhudi, kwa kuwahimiza maofisa wa ngazi zote kutimiza wajibu wao wa kisiasa, kushughulikia matukio makubwa ya uharibifu wa mazingira ya ikolojia na kutatua matatizo mengi makubwa ya mazingira ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi.

Mkutano huo umesisitiza kushikilia na kuimarisha uongozi wa CPC juu ya ukaguzi wa ulinzi wa mazingira, kuendelea kuchukulia kazi ya ukaguzi kama zana yenye nguvu, na kuwajibisha zaidi serikali za mitaa na idara kwa majukumu yao ya kisiasa ya kuendeleza ujenzi wa China yenye Kupendeza.

Umesisitiza umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kushughulikia masuala magumu, kuendelea kufichua na kushughulikia matatizo bila kuyumba, na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa maamuzi na mipango ya Kamati Kuu ya CPC kuhusu ustaarabu wa ikolojia.

“Juu ya ukaguzi wa nidhamu, mkutano huo umesema baadhi ya matatizo yamegunduliwa na timu za ukaguzi zilizokwenda kwenye vyombo na idara kuu za Chama na Serikali. Shida hizi lazima zirekebishwe kwa umakini,” mkutano huo umeongeza.

Mkutano huo umedhihirisha kuwa mwaka 2025 ni muhimu kwa upanuzi wa ukaguzi wa kinidhamu ili kuhusisha maeneo yote, mkutano huo umesema ni lazima mkazo uwekwe katika utekelezaji wa maamuzi na mipango ya Kamati Kuu ya CPC ili kutoa uhakikisho thabiti kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Mkutano huo pia umejadili mambo mengine.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha