Viongozi wa kijeshi kutoka Uganda na DRC wawataka wapiganaji kujisalimisha

(CRI Online) Machi 31, 2025

Viongozi wa kijeshi kutoka Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wametoa wito kwa makundi yenye silaha katika eneo lenye vurugu la mashariki mwa DRC kujisalimisha na kujiunga na mpango wa serikali ya DRC wa kusalimisha silaha.

Chris Magezi, kaimu msemaji wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi la Uganda (UPDF), amesema katika taarifa iliyotolewa jana Jumapili kwamba, makamanda wamewataka wapiganaji wenye silaha kukumbatia mpango wa serikali ya DRC wa kusalimisha silaha, kusambaratisha makundi yao, kuwajumuisha tena katika jamii na kuleta utulivu.

Ameonya kuwa wapiganaji watakaokataa kujisalimisha watalengwa.

Wito huo umetolewa kufuatia mkutano uliofanyika Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri nchini DRC, kuanzia Machi 27 hadi 28, ambao ni sehemu ya operesheni ya pamoja ya kijeshi, inayojulikana kama "Operesheni Shujaa," dhidi ya waasi wa kundi la ADF.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha